array(0) { } Radio Maisha | Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auliwa

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auliwa

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auliwa

Idara ya Upelelezi Nchini DCI imewatuma maafisa kuchunguza kuuliwa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Sharon Otieno.

Kulingana na Mkurugenzi wa DCI  George Kinoti, amesema watahakikisha chanzo cha mauaji hayo na washukiwa wanapatikana ili hatua kali zichukuliwe.

Wakati uo uo, Muungano wa Wanahabari umeitaka serikali kuchunguza kwa haraka kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu aliyetekwa nyara akiwa na mwanahabari wa Nation, Barrack Oduor.

Muungano huo vilevile unataka kisa ambapo mwanahabari huyo alipnea chupuchupu kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa watekaji nyara kuchunguzwa  ili kuwahakikisha wanahabari usalama wanapotekeleza majukumu yao.

Hayo yakjiri, msemaji wa serikali Eric Kiraithe ameahidi kwamba serikali itafanya uchunguzi wa kina kufuatia kisa hicho. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Kiraithe amesikitikia kifo cha Sharon Otieno kadhalika kukiri kwamba kwa sasa ishara zote ni kuwa aliuliwa.

Wakati uo huo, Gavana wa Migori Okoth Obado ameyakashifu madai yanayomhusisha na kutekwa nyara kisha kuuliwa kwa mwafunzi wa Chuo Kikuu, Sharon Otieno. Kulingana na Afisa wa Mawasiliano katika ofisi ya Gavana Obado, Nicholus Anyuor madai hayo ni njama ya kumharibia jina.

Gavana Obado aidha amevitaka vyombo vya habari kukoma kumhusisha na kisa hicho ambacho vilevile kinahusisha kutekwa nyara kwa mwanahabari wa Shirika la Nation, Barack Oduor aliyefanikiwa kutoroka mikononi pa watekaji nyara hao.

Anyuor amedai kisa hicho kinachochewa kisiasa na kuwataka maafisa wa polisi kufanya uchunguzi wa haraka. Kulingana naye, kukamatwa kwa Michael Oyamo aliyetajwa kuwa msaidizi wa gavana hakufai kumhusisha gavana pia.

Mwili wa Sharon ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo umepatikana mapema leo katika Msitu wa Kodera ukiwa na alama za kudungwa visu.