array(0) { } Radio Maisha | Uhuru kuhudhuria kikao cha kongamano la Uchina-Afrika

Uhuru kuhudhuria kikao cha kongamano la Uchina-Afrika

Uhuru kuhudhuria kikao cha kongamano la Uchina-Afrika

Rais Uhuru Kenyatta, Jumatatu anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa bara la Afrika watakoshiriki kongamano la ushirikiano wa Uchina na Afrika linalong'oa nanga rasmi Jumatatu.

Mbali na kushirikia kongamano hilo, Rais Kenyatta ameratibiwa kufanya kikao na Rais wa Uchina, Xi Jinping, mkutano utakaoangazia zaidi uchumi, miundo msingi, uwekezaji, elimu na teknolojia.

Aidha atashuhudia kutiwa saini kwa mktaba wa ushirikiano wa kiuchumi na uwekazaji baina ya Uchina na Kenya.

Mkutano huu unajiri wakati Rais Jinping akisema kuwa miradi inayotelezwa na taifa lake barani Afrika hailengi kujipatia sifa, bali kuimarisha miundo-msingi kwani ndiyo iliyotajwa kuwa kikwazo kikuu cha maendeleo.