array(0) { } Radio Maisha | Seneta wa Baringo, Gideon Moi apinga ongezeko la bei ya mafuta

Seneta wa Baringo, Gideon Moi apinga ongezeko la bei ya mafuta

Seneta wa Baringo, Gideon Moi apinga ongezeko la bei ya mafuta

Seneta wa Baringo, Gideon Moi amesema kuongezwa kwa kodi ya bidhaa za mafuta kwa asilimia 16, kutasababisha gharama ya maisha kupanda zaidi ya ilivyo sasa. Amesema licha ya kuwa serikali inahitaji fedha za kuifadhili miradi ya maendeleo, kuongeza viwango vya kodi kutaathiri ukuaji wa uchumi, kusababisha mfumko wa bei za bidha na hata kusababisha Wakenya wengi kupoteza kazi. 

 Ameishauri serikali na idara nyingine zinazohusika kuzingatia mbinu nyingine za kujipatia pesa badala ya kuwasababishia Wakenya mzigo wa kiuchumi.