array(0) { } Radio Maisha | 'Ndege zinazoelekea na kuondoka Ethiopia si salama' yaonya KATCA

'Ndege zinazoelekea na kuondoka Ethiopia si salama' yaonya KATCA

'Ndege zinazoelekea na kuondoka Ethiopia si salama' yaonya KATCA

Muungano wa Kuthibiti Usafiri wa Angani Kenya Air Traffic Controllers’ Association, umeonya kwamba ndege zinaazoondoka nchini kuelekea Ethiopia na zile zinazoingia nchini kutoka taifa hilo si salama. Rais wa Muungano huo Peter Ang’awa amesema hali hiyo inafuatia mgomo wa wenzao nchini Ethiopia tangu siku ya Alhamisi. Amesema maafisa wa usafiri wa angani wa Ethiopia ambao ni wa muungano huo hawajuwa wakifuata makubaliano ya mawasiano baina ya Kenya na Ethiopia wakati ndege zao zinasafiri kuanzia wiki hii.

Mapema wiki hii Muungano huo Nchini Ethiopia ulitishia kugoma kulalamikia hali mbaya ya mazingira yao ya kufanyia kazi.

Japo washikadau wa usafiri wa angani nchini Ethiopia walisema kuwa mgomo huo hautaathiri usafiri, wenzao nchini Kenya wameomba tatizo hilo kushughulikiwa haraka iwezekanavyo ili kuzuia madhara.