array(0) { } Radio Maisha | Kodi ya 16% kwa bidhaa za mafuta, kuanza kutekelezwa yasema KRA

Kodi ya 16% kwa bidhaa za mafuta, kuanza kutekelezwa yasema KRA

Kodi ya 16% kwa bidhaa za mafuta, kuanza kutekelezwa yasema KRA

Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA imetangaza kuwa utozaji kodi hiyo utaanza kutekelezwa rasmi leo. Aidha  KRA imewapa makataa hadi tarehe 20 mwezi huu wafanyabiashara wa mafuta kuwasilisha stakabadhi zinazoonesha kuwa wamelipia kodi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari KRA imesema itahsirikiana na wafanyabaishara hao kuhakikisha sheria ya ulipiaji kdo ya asilimia 16 inatekelezwa. Aidha imesema itaishirikisha Tume ya Kuthibiti Kawi ERC kufanikisha mpango huo.

 

Hayo yanajiri huku Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi COTU Francis Atwoli akisema kwmaba watalazimika kuwashinikiza wafanyakazi waote kote nchini kushiriki mgomo kupinga hatua hiyo..

Atwoli amemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP Noordin Hajji kumchunguza Waziri wa Fedha Henry Rotich kwa kuagiza kodi hiyo kuanza kutozwa licha ya Bunge la kitaifa kupitisha sheria kusitisha utozaji huo.

Wakati uo huo, Mbunge Maalum Godfrey Otsosi, amemkosoa Waziri Rotich huku akimkashfu kwa kulipuuza bunge.

Hapo jana Waziri  Rotich alisisitiza kuwa huo utatekelezwa kwani tayari ni sheria na sasa kuanzia leo usiku bei ya mafuta na bidhaa nyingi huenda itapanda kwa kiasi kikubwa.

Wabunge siku ya jumataano walisitisha sheria hiyo baada ya kuidhinisha mswada wa mabadiliko katika sheria ya fedha ya mwaka 2018 uliowasilishwa na Kiranja wa Wachache, Junet Mohammed.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye aliondoka nchini kuelekea Uchina leo, hakuwa ametia saini mswada huo uliopitishwa na bunge kuwa sheria.