array(0) { } Radio Maisha | Airgate Mall kubomolewa wiki ijayo

Airgate Mall kubomolewa wiki ijayo

Airgate Mall kubomolewa wiki ijayo

Shughuli  ya ubomoaji jijini  intarajiwa kuendelea wiki ijayo wakati ambapo jumba la Airgate Mall awali Taj Mall litakapobomolewa. Hatua hii itajiri baada ya makataa yaliyowekwa kwa wafanyabishara katika jumba hilo kuondoka kukamilika jana.

Mwenyekiti wa jopo maalum la kushughulikia ubomoaji huo, Moses Nyakiongora na Afisa wa Kaunti ya Nairobi, Julius Wanjau, shughuli hiyo itarajelewa baada ya kukamilisha ubomoaji wa majumba mengine kama vile Southend Mall ambayo licha ya kuanza kubomolewa mapema mwezi huu, sehemu kubwa ingali imara.

Mmiliki wa jumba la Airgate Mall, Ramesh Gorassia amekataa katakata kulibomoa jumba hilo licha ya kuagizwa kufanya hivyo akisisitiza alifuata taratibu zote za kisheria.