array(0) { } Radio Maisha | Serikali kuanza kuwalipa wakulima wa mahindi Septemba 7

Serikali kuanza kuwalipa wakulima wa mahindi Septemba 7

Serikali kuanza kuwalipa wakulima wa mahindi Septemba 7

Kuanzia tarehe 7 Septemba, wakulima wataanza kupokea malipo yao kutokana na mahindi waliyowasilisha kwa serikali msimu uliopita wa mavuno. Waziri wa Ugatuzi, Eugene Wamalwa ameiambia Kamati ya Seneti ya Kilimo kuwa mchujo wa wakulima ulioanza Agosti 20 ili kuwatambua walio halali unakaribia kukamilika kabla ya malipo kuanza kutolewa.

Wamalwa amesema wakulimia 297 ambao tayari wameidhinishwa watakuwa wa kwanza kupokezwa malipo yao.
Aidha amesema wafanyabiashara walaghai watawekwa wazi na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.


Waziri huyo amesema kufikia jana, miongoni mwa wakulima 998 ambao hawajalipwa kwa kuwasilisha mazao yao, ni 317 pekee ambao wamejaza fomu za kuthibitisha uhalali wao huku wengine 723 waliozichukua fomu hizo wakikosa kuzirejesha kwa idara inayohusika.

Jumla ya shilingi bilioni 1.4 zilizotolewa na serikali kuwalipa wakulima zinatarajiwa kufanikisha malipo kwa asilimia 61 ya wakulima. Wamalwa amesema fedha hizo zitakapoisha, wizara itaiomba serikali fedha zaidi ili kukamilisha malipo kwa wakulima.