array(0) { } Radio Maisha | Uingereza yapiga jeki vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya

Uingereza yapiga jeki vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya

Uingereza yapiga jeki vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya

Uingereza imeihakikishia serikali ya Kenya kwamba itashirikiana nayo katika vita dhidi ya ufisadi. Waziri Uingereza Theresa May amesema atahakikisha fedha za umma zilizoibwa na kupatikana kupitia njia haramu kama vile ufisadi na ugaidi na zinazohifadhiwa katika benki nchini humo zitarejeshwa.

Akizipongeza juhudi za Rais Uhuru Kenyatta kukabili ufisadi amesema fedha hizo zitatumika katika kuifadhili miradi ya maendeleo katika sekta za elimu na afya.

Mbali na masuala hayo ya ufisadi, Uingereza pia imesema itaisaidia Kenya kuimarisha vita dhidi ya makundi ya kigaidi hivyo kuimarisha usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuhusu masuala ya biashara, Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema wameafikina kuwa hatua ya Uingereza kujiondoa kwenye Muungano wa Umoja wa Ulaya EU maarufu Brexit haitaathiri ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa haya mawili.

May amerejelea kauli yake alipokuwa  Afrika Kusini kwamba Uingereza inalenga kuipiku Marekani katika uwekezaji Barani Afrika ifikiapo mwaka 2022.