array(0) { } Radio Maisha | Teresa May kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta

Teresa May kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta

Teresa May kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na Rais Uhuru Kenyatta, kwa sasa wanawahutubia wanahabari baada ya kikao kinachoendelea katika Ikulu. Anayehutubu sasa hivi ni Rais Uhuru Kenyatta.

May aliwasili mapema leo leo ikiwa ni siku yake ya mwisho katika zauara ya Bara Afrika. Anapokamilisha ziara yake Barani Afrika anatarajiwa kutangaza makubaliano baina ya serikali yake na idara za usalama nchini, ili kukabili visa vya dhuluma za kimapenzi dhidi ya watoto kupitia mitandao.

Makubaliano hayo aidha yanalenga kuimarisha usalama wa angani kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyoweza kubainisha viliuzi.  Wakati uo huo anatarajiwa kuihakikishia Kenya kwamba serikali yake itahakikisha kuwa fedha za umma zilizoibwa na kupatikana kupitia njia haramu kama vile ufisadi na ugaidi na zinazohifadhiwa katika benki nchini humo zitarejeshwa.

Fedha hizo zitatumika katika kuiafadhili miradi ya maendeleo katika sekta za elimu na afya. Ikumbukwe Kenya huuza bidhaa zake nchini katika masoko ya EU kupitia Uingereza na inahofiwa huenda mpango wake wa kuondoka katika umoja huo ukaathiri shughuli hizo.

Wakati wa Ziara yake Nchini Afrika Kusini May alisema Uingereza inalenga kuipiku Marekani katika uwekezaji Barani Afrika ifikiapo mwaka 2022.

Kwa sasa anafanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta faraghani kabla ya kuwahutubia wanahabari.

Theresa May amewasili humu nchini kwa ziara ya siku moja  alfajiri ya leo.

May amefanya ziara yake ya kwanza Afrika kwa kuzuru Afrika Kusini Nigeria na sasa Kenya.

Kadhalika, May atakuwa ni Waziri Mkuu wa pili wa Uingereza kuzuru Kenya baada ya Margaret Thatcher mwaka 1988. Masuala ya usalama, Raslimali ya maziwa kuu na kurahisisha usafiri ni baadhi ya masuala yatakayopewa kipaumbele.