array(0) { } Radio Maisha | Wakazi Bomet walalamika

Wakazi Bomet walalamika

Wakazi Bomet walalamika

Wakazi Bomet  wamelalamikia kupata maji machafu kupitia mifereji yao kwa muda wa siku tano sasa yaani kuanzia Jumapili. Katika picha ambazo Radio Maisha imeweza kuzipata kadhalika mazungumzo na wakazi, maji hayo yana rangi ya  hudhurungi hali ambayo imewaacha wakazi wengi na wasiwasi kuhusu iwapo wanaweza kuyatumia au la.

Hata hivyo maafisa wa maji katika maeneo ya Longisa na Mulot wamepinga kwamba maji hayo si salama kwa matumizi ya binadamu wakisema ni rangi tu imebadilika kutokana na mvua.