array(0) { } Radio Maisha | Katibu wa Wizara ya Kilimo Richard Lesiyampe akamatwa

Katibu wa Wizara ya Kilimo Richard Lesiyampe akamatwa

Katibu wa Wizara ya Kilimo Richard Lesiyampe akamatwa

Maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi wanaendelea kumhoji Katibu wa Wizara ya Kilimo, Richard Lesiyampe . Lesiyampe ametiwa mbaroni saa chache baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP Noordin Haji kutoa agizo la kukamatwa kwake kufuatia tuhuma za ufisadi katika Bodi ya Mazao na Nafaka. Mwingine aliyetiwa mbaroni ni Mkurugenzi wa NCPB Idara ya Fedha Cornel Kiprotich na Meneja Mkurugenzi wa Bodi ya Mazao na Nafaka NCPB Newton Terer huku wengine tisa wakisakwa.

Uchunguzi katika NCPB ulianzishwa kufuatia madai ya ufujaji wa jumla ya shilingi bilioni 1.9. Uchunguzi wa awali wa Wizara ya Kilimo ulibainisha kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara walioshirikiana na maafisa wa bodi hiyo kuyanunua na kuyauza mahindi kwa bei ya juu huku wakulima wakipuuzwa.

Ripoti ya uchunguzi huo iliwasilishwa mbele ya kamati ya Bunge ya Kilimo na Katibu Lesiyampe.