array(0) { } Radio Maisha | Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kushtakiwa kwa Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kushtakiwa kwa Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kushtakiwa kwa Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda kushtakiwa kwa Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu kufuatia kesi aliyowasilisha katika mahakama hiyo kupinga kushtakiwa kwake. Uamuzi huo umetolewa na Jaji Chacha Mwita.

Mwilu amemshtaki Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji, Mkuu wa Kitengo cha Upelezi, DCI George Kinoti na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Geroge Kinoti kwa madai ya kulenga kumdhalilisha huku akisema DPP hakuwa na mamlaka ya kumtia mbaroni. 

Awali kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo na mahakama kuu, Mahakama ya Milimani imeendeleza vikao vya kesi dhidi ya Mwilu huku mawakili wake wakiongozwa na James Orengo wakisema madai yanayoibuliwa dhidi ya mteja wao yanajenga kumbandua ofisini. Mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu, Lawrence Mugambi, Orengo aidha amelalamikia mwendo wa kasi uliotumiwa kumkamata jana na hata kumwasilisha mahakamani nje ya saa zilizowekwa kisheria.

Orengo aidha amemtaka Mugambi kutokuwa na haraka ya kumtaka Mwilu kukana ama kukubali mashtaka dhidi yake ikizingatiwa tayari wamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu kupinga kushtakiwa kwake katika mahakama hiyo. Orengo  amemtaka Jaji Mugambi kukataa kuisikiliza kesi hiyo kwa misingi kwamba tuhuma zinazoibuniwa dhidi ya jaji Mwilu hazihusu makosa ya uhalifu.

Wakato uo huo upande wa utetezi umedai  kuachwa nje kwa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC katika kushughulikia madai dhidi ya Mwilu ukisema hatua hiyo ni dhihirisho tosha kwamba kuna njama fiche dhidi ya Mwilu.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Mwilu, ni utumizi mbaya wa mamlaka, ukwepaji ulipaji kodi, ufisadi, ukiukaji wa sheria. Jaji Mugambi anatarajiwa kutoa mwelekeo zaidi baadaye leo kufuatia hatua ya Mahakama Kuu kusitisha kwa muda kushtakiwa kwa naibu jaji huyo.