array(0) { } Radio Maisha | Gavana Joho ataka ardhi za umma ziliozonyakuliwa zirudhishwe

Gavana Joho ataka ardhi za umma ziliozonyakuliwa zirudhishwe

Gavana Joho ataka ardhi za umma ziliozonyakuliwa zirudhishwe

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ametoa wito kwa Wakenya na viongozi kwa jumla kushirikiana na serikali kuu na zile za kaunti kuhakilkisha kuwa ardhi za umma zilizonyakuliwa miaka wa awali zinarudhishwa kwa serikali.

Akizungumza mjini Maralal Kaunti ya Samburu Joho amesema kuwa serikali kwa ushirikiano na umma ni lazima ichukue hatua ya kuchukua upya ardhi zilizonyakuliwa na mabwenyebye ili kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vitakuwa na sehemu bora ya kuisha.

Aidha amewaonya watu fisadi wanataumia majina ya watu wengine kuficha mali zao kuwa pia hawatasazwa.

Vilevile amesisitiza haja ya kushirikiana na Rais Uhuru Kenyatta katika kukabili ufisadi akisema kuwa wafanyakazi wa umma wamefanyiwa utathimini wa mali zao bila kuingiza siasa katika suala hilo.