array(0) { } Radio Maisha | Makamishna wa IEBC waliojiuzulu warejea ofisini

Makamishna wa IEBC waliojiuzulu warejea ofisini

Makamishna wa IEBC waliojiuzulu warejea ofisini

Mvutano unatarajiwa kuzuka katika Tume ya Uchaguzi IEBC baada ya makamishna wawili miongoni mwa watatu wlaiojiuzulu kurejea ofisini leo. Utata ulishughudiwa katika ofisi za tume hiyo, zilizoko katika jumba la Aniversery baada ya kuarifiwa kwamba Mwenyekiti Wafula Chebukati alipinga kurejea kazini kwa wawili, hao huku nao wakisalia katika ofisi zao.

Mapema mwezi huu, Mahakama Kuu jijini Niarobi ilitoa uamuzi kwamba makamishna waliojizulu wangali ofisini kwani hawakufuata utaratibu wa kisheria walipofanya hivyo. Makamishna hao ni aliyekuwa Naibu Mwenyekiti, Consolata Nkatha na Makamisha - Margaret Mwachanya na Paul Kurgat. Hata hivyo waliorejea ofisini leo ni Maina na Kurgat.

 Watatu hao walijiuzulu mapema mwaka huu baada ya Chebukati kumpa likizo ya lazima aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba. Aidha ikumbukwe waliushtumu uongozi wa Chebukati wakidai unalemaza shughuli za tume.