array(0) { } Radio Maisha | KNUT yasisitiza mgomo ungalipo

KNUT yasisitiza mgomo ungalipo

KNUT yasisitiza mgomo ungalipo

Shughuli za masomo huenda zikaathirika zaidi, muhula ujao kufuatia misimamo mikali ya idara mbalimbali zinazohusika. Chama cha Walimu Nchini, KNUT kimesisitiza kwamba hakijatangaza kusitishwa kwa mgomo, unaotarajiwa kuanza Septemba Mosi kufuatia mazungumzo baina yake na Tume ya Huduma za Walimu, TSC uliofanyika jana.

Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion amesema hawajaafikiana kuusitisha mgomo huo, kwani TSC haijaahidi kuyashughulikia malalamiko wanayoibua. KNUT inaitaka TSC kuwapandisha vyeo walimu, kuistisha mpango wa kuwahamisha walimu unaoendelea vile vile shughuli ya kutathimini utendakazi wao.

TSC kwa upande wake imekana taarifa kwamba imekubalina na KNUT kwamba itawapandisha vyeo jumla ya walimu elfu thelatini. Afisa wa Mawasiliano wa TSC Kihumba Kimotho amesema bado hawajafanya mazungumzo na KNUT kuhusu suala hilo. Imesema malalamiko yanayoibuliwa na KNUT yatajadiliwa wakati wa mkutano ambao umepangiwa kuandaliwa baina ya Septemba tarehe 30  na tarehe 5 Oktoba jinsi ilivyopangwa.

Kwa sasa mpango wa kuwahamisha walimu na kuwafanyia tathmini ya utendakazi unaendelea.