array(0) { } Radio Maisha | Usafirishaji mafuta ghafi kutoka Turkana hadi Mombasa warejelewa

Usafirishaji mafuta ghafi kutoka Turkana hadi Mombasa warejelewa

Usafirishaji mafuta ghafi kutoka Turkana hadi Mombasa warejelewa

Hatimaye shughuli ya usafirishaji mafuta ghafi kutoka Turkana hadi Mombasa imerejelewa rasmi. Shughuli hiyo ilikuwa imesitishwa kwa takribani siku hamsini baada ya wakazi kuitatiza wakilalama kwamba hawanufaiki kiuchumi.

Waziri wa Mafuta na Madini, John Munyes na viongozi wengine tayari wamefanya zaidi ya mikutano mitano kwenye kaunti ndogo za Turkana Mashariki na Turkana Kusini Kurai wakazi kutotatiza usafirishaji wa mafuta.

Wakati uo huo, Mbunge wa Turkana Kusini, James Lomenen amesema mapato ya mafuta yanafaa kuwanufaisha wenyeji.

 

Leo asubuhi, malori ya mafuta yalianza kusafirisha mafuta kwenda Mombasa, yakiwa yamebeba jumla ya mapipa mia sita ya mafuta huku mengine milioni mia saba hamsini yakiwa tayari kusafirishwa.

Tayari serikali imeitikia wito wa wakazi kwa kuwapeleka maafisa wa usalama wa kutosha eneo la Lokori ambapo utovu wa usalama ulikuwa umekitiri.