array(0) { } Radio Maisha | Wetangula arekodi taarifa kuhusu kisa cha shambulizi wakati wa mazishi

Wetangula arekodi taarifa kuhusu kisa cha shambulizi wakati wa mazishi

Wetangula arekodi taarifa kuhusu kisa cha shambulizi wakati wa mazishi
Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula amerekodi taarifa katika makao makuu ya polisi mjini Kitale kuhusu kisa ambapo watu watano walijeruhiwa wakati wa mazishi eneo la Kiminini. Wetangula amesisitiza kuwa asingependa kisa kama hicho kishuhudiwe tena na kuwa watakaopatikana na hatia ya kutekeleza uovu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
 
Hayo yanajiri siku moja tu baada ya Mbunge wa Likuyani, Daktari Enock Kibunguchi kurekodi taarifa katika kituo hicho cha polisi ili kueleza anachokifahamu kuhusu kisa hicho.
 
Siku ya Jumanne, Kamanda wa Polisi kaunti hiyo, Samson Ole Kine aliwaagiza walinzi wote wa viongozi waliokuwa kwenye mazishi hayo kuripoti mara moja katika makao makuu hayo kuwasilisha silaha wanazomiliki na kurekodi taarifa.
 
Walinzi walioagizwa ni Mbunge Eseli Simiyu waTongereni, Wafula Wamunyinyi wa Kanduyi, Vincent Kemosi wa Mugirango Magharibi na Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula.