array(0) { } Radio Maisha | Bobi Wine akamatwa tena
Bobi Wine akamatwa tena

Dakika chache baada ya Mahakama ya Kijeshi Nchini Uganda kumwondolea mashtaka Mbunge Robert Kyangulani maarufu Bobi Wine, Mbunge huyo amekamatwa tena. Bobi Wine amekamatwa na kupelekwa katika mahakama ya kiraia ya Gulu nchini Uganda ambapo anatarajiwa kushtakiwa kwa tuhuma za uhaini.

Bobi Wine ambaye alionekana kuwa mnyonge na asiyeweza kutembea bila usaidizi amepelekwa katika mahakama hiyo akiwa ameandamana na mkewe pamoja na mawakili wake, ambao pamoja na mshukiwa wamesema wako tayari kushirikiana na serikali bila mvutano wowote.

Hayo yanajiri huku Maafisa nchini humo wakimkamata Kiongozi wa Upinzani nchini humo Kizza Besigye. Besigye amekamatwa alipoaribu kuondoka nyumbani wake eneo la Kasangati, na amepelekwa katika kituo cha polisi cha Naggalama ambapoa nazuiliwa.

Ikumbukwe awali polisi walishika doria nyumbani kwake pamoja na kwa Katibu wa Kitaifa wa Chama cha Forum for Democratic Change Ingrid Turunawe, na Meya wa Wakaliga Erias Lukwago.

Kulingana na Turinawe polisi walifika nyumbani kwake asubuhi mwendo wa saa kumi na moja na kumzuia mwanawe kuondka. Amesema hajaelezwa ni kwa nini polisi walitumwa nyumbani kwake, kushika doria.