array(0) { } Radio Maisha | Bobi Wine aachiliwa huru
Bobi Wine aachiliwa huru

Hatimaye, Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imemwondolea mashtaka ya umiliki wa silaha kinyume na sheria Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maaruf Bobi Wine.

Hata hivyo, mahakama hiyo imeagiza Bobi kukabidhiwa kwa maafis wa polisi wa Uganda ambao wanatarajiwa kumfungulia mashataka ya uhaini yani treason.

Kuondolewa kwa makosa dhidi yake kunajiri wakati wanaharakati na wanasheria humu nchini wakiwa tayari wamekusanyika katika eneo la Freedom Corner, kwenye Bustani ya Uhuru kwa maandamano ya kupinga kukamatwa kwa Bobi.