array(0) { } Radio Maisha | Kesi ya ufisadi inayomkabili Kidero yaahirishwa

Kesi ya ufisadi inayomkabili Kidero yaahirishwa

Kesi ya ufisadi inayomkabili Kidero yaahirishwa

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Evans Kidero na baadhi ya maafisa wa kaunti hiyo watafikishwa tena mahakamani tarehe sita mwezi ujao wakikabiliwa na kesi ya utumiaji mbaya wa madaraka kuahirishwa hadi tarehe sita mwezi ujao baada ya upande wa mashtaka kukosa kuwasilisha mahakamani ushahidi wa kutosha.

Hakimu Justice Mugambi amekiri kutopokea ushaidi kutoka kwa maafisa wa EACC, hivyo kumwachilia kidero na mwenzake kwa dhamana ya fedha taslim milioni mbili kila mmoja huku washukiwa wengine wakipewa dhamana ya mali yenye thamani ya shilingi milioni tano.

Kidero na baadhi ya maafisa wa zamani wa kaunti hiyo, wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababaishia serikali ya Kaunti ya Nairobi hasara ya takriban shilingi milioni 231 kukiwamo kutoa kandarasi ghushi kwa watu wasiojulikana.

Mapema mwezi huu mahakama inayoshughulikia kesi za ufisadi ilimwachilia Kidero kwa dhamana ya shilingi milioni mbili pesa taslim baada ya kufikishwa mahakamani pamoja na aliyekuwa msimamizi wa fedha wa kaunti akiwa uongozini.