array(0) { } Radio Maisha | Polisi wanasa sukari na sigara zinazodaiwa kuingizwa nchini kimagendo

Polisi wanasa sukari na sigara zinazodaiwa kuingizwa nchini kimagendo

Polisi wanasa sukari na sigara zinazodaiwa kuingizwa nchini kimagendo

Maafisa wa polisi wamenasa tani thelathini na sita za sukari na konteina mia sita tisini na moja za sigara . Bidhaa hizo zimenaswa mjini Wajir na Lokichar na zinaaminika  kuingizwa nchini kutoka mataifa ya Somalia na Sudan.

Hayo yanajiri huku serikali ikisema kwamba Maafisa wa Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa nchini KEBS watahojiwa ili kukabili tatizo la kuingizwa nchini bidhaa kimagendo na ambazo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Wakati uo huo, Wizara ya Viwanda imekana taarifa kwamba kuna madini ya zebaki yaa ni Mercury na Shaba, katika sukar inayouzwa nchini. Waziri Peter Munya amesema ripoti kuhusu madai hayo iliyotolewa awali si ya kweli. Aidha amesema magunia laki tatu ya sukari inayoaminika kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu yataharibiwa.

Wakati uo huo, amesema kwamba Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa Nchini KEBS linaendelea na kutathimini bidhaa zinazoingizwa humu nchini kuhakikisha kuwa zinaafikia viwango vinavyohitajika na ni salama kwa matuizi ya binadamu kabla ya kuanza kuuzwa katika masoko ya humu nchini.

Mbali na sukari, Munya amesema wamenasa magunia ya mbolea na mchele bidhaa zinazodaiwa kuwa si salama. Amesema mchele huo ungali unazuiliwa na uchunguzi unaendelea.

Hata hivyo, amesema uchunguzi wa awali kuhusu mbolea umekamilika, na itaharibiwa hivi karibuni.