array(0) { } Radio Maisha | Kadhi Mkuu awashtumu wanaokosoa maamuzi yake

Kadhi Mkuu awashtumu wanaokosoa maamuzi yake

Kadhi Mkuu awashtumu wanaokosoa maamuzi yake

Kadhi mkuu nchini Ahmed Muhdhar amesema kamwe hatayumbishwa na wanaomshtumu kwa kutangaza leo kuwa maadhimisho ya sherehe za Idi Ul Adha kinyume na tangazo la Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i kwamba sherehe hizo zifanyike jana.

Akizungumza wakati wa kuongoza swala ya Siku ya Eid Ul Adh'a katika Uwanja wa Shule ya Msingi ya Ronald Ngala jijini Mombasa, Muhdhar amesema utendakazi wake umekuwa ukiambatana na sheria za Dini ya kislamu. Amewahimiza waislamu kusalia imara na kuepuka mgawanyiko wa aina yoyote.

Kwa upande wake kadhi wa zamani, Khamad Kassim amemkosoa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Adan Duale kwa kutoa matamshi makali dhidi ya Muhdhar akisema kiongozi huyo hakustahili kutoa matamshi kama hayo.

Shutma zaidi dhidi ya Duale na Waziri wa Utalii, Najib Balala zimeendelezwa na viongozi wa dini ya Kislamu eneo la bonde la ufa wakiongozwa na mwenyekiti wao wa baraza la Maimamu la CIPK Abubakar Bini.

Aidha wamepinga pendekezo la ofisi ya mshauri mkuu wa dini ya Kislamu kwa jina  Mufti kubuniwa huku wakishikilia kwamba majukumu hayo tayari yapo chini ya mamlaka ya chifu kadhi.