array(0) { } Radio Maisha | #FreeBobiWine Wakenya kuandamana siku ya Alhamisi

#FreeBobiWine Wakenya kuandamana siku ya Alhamisi

#FreeBobiWine Wakenya kuandamana siku ya Alhamisi

Maandamo ya amani yataandaliwa siku ya Alhamisi tarehe 23 mwezi Agosti katika ukumbi wa Freedom Corner kupinga kukamatwa kwa Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maaruf Bobi Wine.

Akitoa ratiba kamili katika mtandao wake wa Twitter, Mwanaharakati Boniface Mwangi amesema siku ya Jumatano tarehe 22 mwezi Agosti saa kumi na moja  jioni kutakuwa na tamasha iitwayo Freedom Concert katika ukumbi wa PAWA254,kisha siku ya Alhamisi maandamano yataanza saa tatu katika ukumbi wa Freedom Corner hadi Ubalozi wa Uganda eneo la River Side Drive jijini Nairobi.

Hapo jana, waandamanaji kwenye mpaka wa Kenya na Uganda eneo la Busia, walifunga barabara wakishinikiza kuachiliwa huru kwa Wine. Hali hiyo ilitatiza usafiri wa matrela yanayoingia na kutoka humu nchini.

Bobi alikamatwa mapema wiki jana na inaarifiwa kuwa alijeruhiwa vibaya mikononi pa polisi kiasi cha kutoweza kuongea wala kutembea.

Katika mitandao ya kijamii, alama ya reli FreeabaobiWIne imetumika kuanzia wiki jana kuhamasisha kuachiliwa kwake. Bobi alikamatwa kwa tuhuma za uhaini.