array(0) { } Radio Maisha | Kofi Anna aaga dunia
Kofi Anna aaga dunia

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Anan amefariki dunia. Umoja wa Mataifa umethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo  ambaye alikuwa mpatanishi mkuu humu nchini baada ya ghasia zilizoshughudiwa nchini baada ya  uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.  Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga ametaja kifo cha Annan kuwa pigo kubwa kwa bara hili.

Kulingana na jamaa zake amefariki dunia  nchini Uswizi baada ya kuugua kwa muda mfupi, huku wakisema mipango ya maandalizi itatangazwa baadaye. Annan alikuwa ni Mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.

 

 

Kofi Atta Anan alizaliwa Aprili 8 mwaka 1938 eneo la Kumasi nchini Ghana .  Alisomea chuo cha Macalester ncgini Geneva . Alijiunga na Umoja wa Mataifa mwaka 1962 akihudumu katika ofisi ya Shirika la Afya Duniani WHO. Aidha baina ya mwaka 1992 na Desemba mwaka 1996 alihudumu katika vitengo mbalimbali katika umoja huo.

Tarehe 13 mwezi Desemba mwaka 1996 alichaguliwa kuwa katibu Mkuu wa Umoja huo, ikiwa mara ya kwanza kwa mfanyakazi wa UN kuchaguliwa katika wadhfa huo.Alihudumu katika wadha wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataia tangu mwaka 1997 hadi Desemba mwaka 2006. Mwaka 2001 alipokea tuzo ya Amani ya Nobel . Aidha Ndiye mwanzilishi na alikuwa Mwenyekiti wa  wakfu wa Anna Foundation

Alichaguliwa kwa mara ya poli mwaka 2001. Nafasi hiyo ilichukuliwa na Ban Kim- Moon mwaka 2007. Mwaka 2012 Anna alikuwa miongoni mwa kundi na UN kuhusu mataifa ya kiarabu lililoteuliwa kutafuta suluhu ya vita nchini Syria. Hata hivyo alijiondoa baada ya kudai ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa UN katika kutafuta suluhu. Septemba mwaka 2016 alichaguliwa na Tume ya Kimataifa kuchunguza mzozo nchini Rohingya.

Akiwa Katibu mkuu mataifa yalikumbwa n achangamoto nyingi mfano; vita nchini Iraq na janga la virusi vya HIV na Ugonjwa wa ukimwi.

Amefariki dunia mapema Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nchini Switzerland . Alikuwa na miaka 80.