array(0) { } Radio Maisha | Kidero akana mashtaka ya ufisadi dhidi yake

Kidero akana mashtaka ya ufisadi dhidi yake

Kidero akana mashtaka ya ufisadi dhidi yake

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero amekana mashtaka ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili. Kidero ambaye alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya ufisadi Douglas Ogoti pamoja na aliyekuwa afisa wa fedha kaitka kaunti yake Maurice Okello, anatuhumiwa kuhusika katika ufujaji wa shilingi bilioni mia mbili kumi na tatu 213.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP aliiomba mahakama kutowaachilia kwa dhamana washukiwa hadi pale kesi dhidi yao itakaposikilizwa na kuamuliwa. Kulingana DPP iwapo Kidero na Wenzake wangeeachiliwa huenda wangeingilia uchunguzi kuhusu kesi zinazowakabili.

Hata hivyo, mawakili wa Kidero walipinga ombi hilo wakisema meja wao ana haki ya kuachiliwa kwa dhamana kwnai mashtaka dhidi yao hayajadhibitishwa. Vile vile waliiomba mahakama kutoendelea kuwazuilia washukiwa kwani hatua hiyo ni ukiukaji wa haki zao. Peter Wayama ni mmoja wa washukiwa.

Ikumbukwe Kidero alikamatwa jana na maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC kwa tuhuma za ufijaji wa pesa na utumizi mbaya wa mamlaka wakati akihudumu katika wadhfa wa ugavana. Kukamatwa kwa Kidero kulifuatia agizo lililotolewa na DPP.