array(0) { } Radio Maisha | Mutua afanya uteuzi wa maafisa wa kaunti

Mutua afanya uteuzi wa maafisa wa kaunti

Mutua afanya uteuzi wa maafisa wa kaunti

Siku chache baada ya kuwaidhinisha mawaziri wake kuanza kuhudumu bila idhini ya bunge la kaunti, Gavana wa Machakos, Alfred Mutua amewateua maafisa wakuu 29 katika kila wizara ya kaunti, vilevile washauri wakuu wa vitengo vitatu maalum.

Akiwahutubia wanahabari mjini Machakos, Mutua amesema alizingatia sheria za uteuzi wa maafisa wakuu na wote ambao amewateua, wamekaguliwa kwa kuzingatia namna walivyofuzu katika taaluma mbalimbali.


Mutua aidha amewaomba wawakilishi wadi wa Kaunti ya Machakos kuwakagua vyema maafisa hao anaolenga wafanikishe zaidi maendeleo katika kaunti hiyo.

Miongoni mwa maafisa walioteuliwa ni aliyekuwa mgombea useneta kwenye kaunti hiyo, Carlos Kioko ambaye ameteuliwa kuhudumu katika Wizara ya Vijana na Michezo, aliyegombea ubunge wa eneo la Kangundo, Ancent Kituku Nzioka akiteuliwa kuwa mshauri maalum katika Wizara ya Afya huku maafisa watano wakiteuliwa kwa mara ya pili, miongoni mwa wengine.