array(0) { } Radio Maisha | Kalonzo akutana na Wetangula kujadili hatma ya NASA

Kalonzo akutana na Wetangula kujadili hatma ya NASA

Kalonzo akutana na Wetangula kujadili hatma ya NASA

Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka ameanza kutekeleza ahadi yake ya kuwa mpatanishi wa Raila Odinga wa ODM na Moses Wetangula wa Ford - Kenya, ambapo leo amefanya mkutano na Wetangula katika makao makuu ya chama chake.

Wiki iliyopita, Musyoka alitangaza kujitolea kwake kuwapatanisha wawili hao ambao wamekuwa wakirushiana cheche za maneno, hasa kuhusu hatima ya muungano wa NASA.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Musyoka amesisitiza kuwa ataendeleza juhudi za kufanikisha mshikamano wa vyama tanzu vya NASA, akishikilia kwamba umoja wao utafanikisha ukuaji wa taifa na uwapo wa amani.

Kwa upande wake, Wetangula amesema chama chake na kile cha Wiper vina ajenda moja, hivyo wataendeleza umoja.

Wiki mbili zilizopita, Wetangula alitangaza kuwa NASA haina umaarufu tena na kuwa amejitenga kabisa na muungano huo, wala hatashirikiana tena na Raila, matamshi yaliyowaghadhabisha wabunge wa ODM na kumtaka kuwarai viongozi wa Ford-Kenya kujiondoa katika nyadhifa wanazoshikilia bungeni.