array(0) { } Radio Maisha | Chama cha ODM kuwaadhibu wabunge waasi

Chama cha ODM kuwaadhibu wabunge waasi

Chama cha ODM kuwaadhibu wabunge waasi

Chama cha ODM, kimewaonya Mbunge wa Msambweni na mwenzake wa Malindi, Aisha Jumwa kufuatia matamshi yao ya hivi karibuni dhidi ya chama hicho na uongozi wake.

Katika barua iliyoandikiwa wawili hao juma lililopita, walipewa makata ya siku saba yanayokamilika leo kueleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua.

Mwenyekiti wa ODM, John Mbadi amewakashifu wabunge hao wa Pwani kwa kuendelea kukiuka sheria za vyama vya kisiasa pamoja na katiba ya ODM.

Jumwa anashtumiwa kwa kutoa matamshi ya uongo dhidi ya kiongozi wa chama hicho, Raila Odinga. Aidha anadaiwa kuvunja mkataba baina yake na chama hicho ambacho alikitumia kuingia bungeni.

Barua hiyo inaashiria kuwa ODM imeanza kuwachukulia hatua wale wanaopinga misimamo yao na kujiunga na vyama pinzani.