array(0) { } Radio Maisha | Mahakama kutoa hukumu ya mrembo wa Gereza la Lang'ata baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe

Mahakama kutoa hukumu ya mrembo wa Gereza la Lang'ata baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe

Mahakama kutoa hukumu ya mrembo wa Gereza la Lang'ata baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe

Mahakama Kuu Alhamisi wiki ijayo Julai 19 itatoa hukumu kwa msichana kwa jina Ruth Kamande aliyechaguliwa kuwa Mrembo wa Gereza la Wanawake la Lang'ata mwaka 2016, baada ya kupatikana na hatia ya kumuu mpenziwe. Jaji Jessie Lessit anatarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya Kamande ambaye alimuua Farid Mohames kwa kumdunga kisu mara kadhaa mwaka 2015.

Mahakama ilielezwa kuwa Kamande ambaye alikuwa na umri wa miaka 21 alipotenda kitendo hicho kwamba anajutia makosa yake. Mawakili wake vilevile walisema amekuwa akizuiliwa kwa miaka miwili na miezi tisa, muda ambao umemsaidia kubaidili tabia.

Aidha inaarifiwa kuwa amekuwa akipewa mafunzo ya dini na masuala mengine ikiwa njia mojawapo ya kukuza imani yake.