array(0) { } Radio Maisha | Seneti yadai kuwapo njama fiche kwenye uchunguzi wa Solai

Seneti yadai kuwapo njama fiche kwenye uchunguzi wa Solai

Seneti yadai kuwapo njama fiche kwenye uchunguzi wa Solai

Katibu wa Utawala katika Wizara wa Masuala ya Ndani, Patrick Ole Ntutu ameahidi kuchunguza madai kwamba serikali imeanza mikakati ya kuwafidia waathiriwa wa mkasa wa bwawa la Solai wakati ambapo mshukiwa mkuu Manskhul Patel anaendelea kukabiliwa na kesi mahakamani.

Akizungumza alipofika mbele ya Kamati Maalum ya seneti inayochunguza mkasa huo Ntutu amesema wizara yake hiahusiki katika fidia hiyo licha ya madai kwamba Kamishna wa Nakuru ameanza kusambaza karatasi zinazojazwa na waathiriwa.

Akiuliza maswali wakati wa vikao hivyo, mmoja wa wanachama wa kamati hiyo, Mutula Kilonzo Jnr amesema hatua hiyo huenda ikahujumu miakakati ya kuwajibisha waliohusika mahakamani kadhalika kuwapo njama fiche ya kuwafidia wasiostahili kufuatia madai zaidi kwamba kuna orodha tofauti tofauti zinazotumika kutayarisha fidia. 

Wanachama wa kamati hiyo vilevile wamedai kupokea vitisho lakini kuahidi kutoumbishwa katika azma ya kuwahakikishia haki waathiriwa. 

Maafisa wengine wa serikali katika kaunti hiyo sasa wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ambayo inawajumuisha maseneta, Johnson Sakaja, Ephram Maina, Susan Kihika, Malachi Ekai, Fatuma Dullo na Sylvia Kasanga.