array(0) { } Radio Maisha | Raila Odinga asisitiza msimamo wake katika vita dhidi ya ufisadi

Raila Odinga asisitiza msimamo wake katika vita dhidi ya ufisadi

Raila Odinga asisitiza msimamo wake katika vita dhidi ya ufisadi

Kinara wa ODM, Raila Odinga amesisitiza msimamo wake katika vita dhidi ya ufisadi na kusema ushirikiano wake na Rais Uhuru Kenyatta utahakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Akiwahutubia wakazi mjini Kitui leo alasiri, Raila amewashtumu wanaoingiza sukari kimagendo nchini, akisema wana lengo la kusambaratisha viwanda vya sukari.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka ambaye amewaomba Raila na Uhuru kushirikiana kukabili ufisadi, akirejelea ahadi waliotoa wakati wa kampeni kwamba watakabili uovu huo.

Kwa upande wake, Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana amewashauri viongozi wote kuungana na kushirikiana katika kufanikisha miradi ya maendeleo ili kuwafaa wananchi. Aidha amepongeza ushirikiano wa Rais na Raila akisema ni mfano unaofaa kuigwa. Viongozi wengine waliokuwapo ni Gavana wa Kitui Charity Ngilu, Naibu wake Wathe Nzau, wabunge wa kaunti hiyo na aliyekuwa mgombea ugavana wa Machakos, Wavinya Ndeti miongoni mwa wengine.