array(0) { } Radio Maisha | Maafisa katika Kaunti ya Busia walioshtakiwa pamoja na Gavana Sospeter Ojaamong wamewasilisha kesi mahakamani kusitisha hatua ya kusimamishwa kazi

Maafisa katika Kaunti ya Busia walioshtakiwa pamoja na Gavana Sospeter Ojaamong wamewasilisha kesi mahakamani kusitisha hatua ya kusimamishwa kazi

Maafisa katika Kaunti ya Busia walioshtakiwa pamoja na Gavana Sospeter Ojaamong wamewasilisha kesi mahakamani kusitisha hatua ya kusimamishwa kazi

Maafisa wakuu katika Kaunti ya Busia ambao walishtakiwa pamoja na Gavana Sospeter Ojaamong kwa madai ya utumiaji mbaya wa ofisi na ukiukaji wa sheria za ununuzi, wamewasilisha kesi katika Mahakama ya Uajri na Leba kusitisha hatua ya kusimamishwa kazi.

Watatu hao Alan Omachari, Samuel Ombui na  Bernard Yaite, kupitia wakili wao Danstan Omari wanadai kuwa Kaunti pamoja na Bodi huduma zake wanapanga kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sehemu ya 62 ya sheria ya Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi, ambayo imesema kwamba afisa anayekabiliwa na makosa hayo anafaa kuondoka ofisini hadi kesi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Wakili Omari anasema sheria hiyo inawabagua watatu hao kwani Gavana Ojaamong ambaye wameshtakiwa pamoja atasalia ofisini wakati kesi yao itakapokuwa ikiendelea. Jaji Bryan Ongaya ameagiza nakala za kesi zikabidhiwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Serikali ya Kaunti ya Busia na Bodi ya Huduma za kaunti. Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 12 Julai mwaka huu.