array(0) { } Radio Maisha | Martha Karua awasilisha kesi mahakamani kwa mara ya tatu kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru

Martha Karua awasilisha kesi mahakamani kwa mara ya tatu kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru

Martha Karua awasilisha kesi mahakamani kwa mara ya tatu kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru

Kiongozi wa Chama cha Narc-Kenya Martha Karua amewasilisha kesi nyingine kwa mara ya tatu mahamani kupinga ushindi wa Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita. Karua amewasilisha kesi mapema leo katika Mahakama ya Rufaa mjini Nyeri licha ya Mahakama Kuu awali kutupilia mbali kesi hiyo mara mbili.

Kesi hiyo ilitupiliwa mbali tarehe 14 mwezi Juni mwaka huu na Jaji Lucy Gitari kwa misingi kwamba haikuwa na uzito na kumuagiza kulipa shilingi milioni tano kugharimia kesi hiyo. Aidha mnamo tarehe 15 mwezi Novemba, mwaka uliopita, Jaji yuyo huyo alitupilia mbali kesi ya Karua akisema haikuwa na ushahidi wa kutosha.

Baadaye aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Rufaa ambayo iliagiza kesi hiyo isikilizwe tena katika Mahakama Kuu. Wakitoa uamuzi wao majaji Mohammed Warsame, Daniel Musinga na William Ouko waliukosoa uamuzi wa kudumisha ushindi wa Waigurur wakisema kesi hiyo ilifutiliwa mbali bila ya yeye kusikilizwa.