array(0) { } Radio Maisha | Wakazi wa mtaa wa Kibera hawatafidiwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya Ngong-Kungu Karumba-Lang’ata

Wakazi wa mtaa wa Kibera hawatafidiwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya Ngong-Kungu Karumba-Lang’ata

Wakazi wa mtaa wa Kibera hawatafidiwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya Ngong-Kungu Karumba-Lang’ata

Wakazi wa mtaa wa Kibera hawatafridiwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya Ngong Road-Kungu Karumba-Lang’ata. Uamuzi huo umetangazwa mapema leo na Tume ya Kitaifa ya Ardhi NLC, Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadamu KNCHR na Mamlaka ya Barabara Kuu Nchini KURA. Tume hizo mbili zimesema kuwa ardhi hiyo ni ya serikali na kwamba mradi huo utaendelea ilivyopangwa. Naibu Mwenyekiti wa NLC Abigael Mbagaya amesema wamiliki wa majumba ambayo yako katika shamba hilo la ekari kumi pekee ndio watakaofidiwa.

Kauli yake imeungwa mkono na Mwenyekiti wa KNCHR Kagwiria Mbogori ambaye amepuuza madai kuwa mradi huo utaiathiri ardhi ya ekari 288 iliyotolewa kwa watu wa jamii ya Wanubi. Naibu Mkurugenzi wa KURA anayehusika na masuala ya majumba Mhandisi Tomothy Nyamboi amesema wamepewa jukumu la kuutekeleza mradi huo wa shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari kwenye barabara za Mbagathi, Ngong ma Lang'ata. Nyamboi ameyasema hayo wakati wa mkutano wa washikadau kati ya KURA, KNCHR, NLC na wakazi.

Wiki iliyopita serikali iliwapa wakazi wa eneo hilo wiki mbili kuondoka kutoa nafasi kwa ujenzi huo kuendelea. Wakazi wa vijiji vya Mashimoni, Lindi, Kambi Muru na Kisumu Ndogo ndio watakaoathirika.