array(0) { } Radio Maisha | Mwanamke aliyekamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa shilingi milioni 140 jijini Dubai afikishwa mahakamani

Mwanamke aliyekamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa shilingi milioni 140 jijini Dubai afikishwa mahakamani

Mwanamke aliyekamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa shilingi milioni 140 jijini Dubai afikishwa mahakamani

Mwanamke mwenye umri wa makamo aliyekamatwa jana kwa kuhusishwa na wizi wa shilingi milioni 14O jijini Dubai amefikishwa mahamani leo. Upande wa mashtaka umeiomba mahakama kuwaruhusu polisi kumzuiliwa Rebacca Musau kwa muda wa wiki mbili ili wakamilishe uchunguzi.

Hata hivyo mahakama haikutoa agizo hilo kwani wakili wa mashukiwa hakuwapo mahakamani. Suala hilo liyasikilizwa kesho na maelekezo kutolewa kuhusu ombi hilo. Mshukiwa atasalia rumande katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga. 

Mshukiwa aliwapeleka maafisa wa upelelezi nyumbani kwake jijini Nairobi baada ya kukamatwa alipokuwa akijaribu kutorokea nchini Tanzania, ambapo polisi walipata shilingi milioni kumi na tatu.