array(0) { } Radio Maisha | Maafisa wawili wanaotuhumiwa kwa kumuua raia wa Uingereza kuzuiliwa rumande

Maafisa wawili wanaotuhumiwa kwa kumuua raia wa Uingereza kuzuiliwa rumande

Maafisa wawili wanaotuhumiwa kwa kumuua raia wa Uingereza kuzuiliwa rumande

 

Maafisa wawili wanaotuhumiwa kwa kumuua mwanmume mmoja raia wa Uingereza Alexander Monsoon, watazuiliwa kwa wiki mbili katika gereza la Shimo la Tewa jijini Mombasa baada ya kunyimwa dhamana na Mahakama Kuu ya Mombasa.

Mapema leo wawili hao Naftali Chege na Ishamel Baraka, wanaohudumu katika kaunti za Nandi na Kisumu, walikana mashtaka ya mauaji dhidi yao. Jaji Erick Ogolla alisema wawili hao watazuiliwa rumande hadi tarehe 19 mwezi huu, wakati ombi lao la kuachiliwa kwa dhmana litakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mshukiwa wa tatu Charles Wangombe Munyiri, hata hivyo aliachiliwa kutokana na hali yake afya. Mahakama imearifiwa kwamba anaugua ugonjwa wa shinikizo la damu, Hypertension na anastahili kumwona daktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta siku ya Jumatatu na Alhamisi ya kila wiki.

Watatu hao ni miongoni mwa watu wanne wanaotuhumiwa kwa kumuua Alexander mnamo mwezi Mei mwaka 2012. Agizo la kukamatwa kwa mshukiwa wa nne John Pamba, ambaye anahudumu katika Kituo cha Polisi cha Diani lilitolewa, lakini akakosa kufika mahakamani leo.