array(0) { } Radio Maisha | Matiang'i ahojiwa na bunge kuhusu bidhaa za magendo

Matiang'i ahojiwa na bunge kuhusu bidhaa za magendo

Matiang'i ahojiwa na bunge kuhusu bidhaa za magendo

Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i amekiri kuwapa kwa matatizo katika ukaguzi wa bidhaa zinaozingizwa nchini maeneo ya mipakani hali inayochangia ongezeko la bidhaa za magendo. Matiang'i hata hivyo amesema wizara yake inaendelea kuweka mikakati mbalimbali kudhibiti hali.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Usalama ambapo alihitajika kutoa sababu ya ongezeko la bidhaa zinazoingizwa nchini kimagendo, Matiang'i amesema changamoto hasa zimetokana na hatua ya wahalifu wanaohusika biashara hizo haramu kubadilisha mtindo wa kuendeleza biashara hizo kila kuchicha.

 Matiang'i hata hivyo amesema wizara yake inaendelea kuweka mikakati ya kudhibiti hali huku akiahidi kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu uagizaji wa bidhaa mbalimbali zikiwamo sukari, mchele na mafuta ya kupikia kinyume na sheria.


Wakati uo huo amekana dhana kwamba huenda wizara yake haishirikiani na idara nyingine za serikali katika vita dhidi ya biashara ya magendo.


Hata hivyo mmoja wa wabunge amesema vita dhidi ya bidhaa za magendo havitafaulu iwapo wahusika wakuu wa biashara hizo hawatatiwa mbaroni. Aidha amesema Waziri wa Fedha, Henry Rotich ni miongoni mwa wanaostahili kuwajibishwa kufuatia kuingizwa kwa sukari nchini ambayo si salama kwa matumizi ya binadama akisema ndiye aliyetoa idhini ya kuagizwa kwa sukari. Kufikia sasa watu 72 wametiwa mbaroni kwa kuhusishwa na uingizaji nchini wa bidhaa mbalimbali kwa njia za magendo.