array(0) { } Radio Maisha | Mkuu wa Mashtaka aagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Bwawa la Patel

Mkuu wa Mashtaka aagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Bwawa la Patel

Mkuu wa Mashtaka aagiza kukamatwa kwa mmiliki wa Bwawa la Patel

 

Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP, Noordin Haji ametoa agizo la kukamatwa na kushtakiwa kwa maafisa wa Bwawa la Solai, Mamlaka ya Raslimali za Maji WRA na wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Mazingira NEMA kufuatia mkasa uliosababisha vifo ya watu arubaini na wanane baada ya maji kuvunja kuta za bwawa hilo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Haji amesema uchunguzi uliofanywa kufuatia mkasa huo ulibaini kuwa bwawa hilo lilijengwa na watua ambao hawakuhitimu na kwa kutumia vifaa vya shamba hilo. Vilevile ilibainika kuwa maji ya bwawa hilo yalikuwa yakiwekwa na kampuni kwa jina Watkins Stream na kwamba leseni ya maji hayo ilitolewa kinyume na sheria. Kadhalika DPP amesema WRA, NEMA pamoja na mmiliki Perry Mansukh hawakutekeleza majukumu yao ya kuhakikisha sheria za mazingia zinazingatiwa.

Kufuatia hali hiyo Haji amesema kuna ushahidi wa kutosha kuwashtaki Perry Mansukh Kansagara, mmiliki wa Bwawa la Solai, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Patel Coffe Estates Vinoja Kumar, maafisa wa WRA Winnie Muthoni Mutisya, Tomkin Odo Odhiambo na Jecinta Were, pamoja na  Willice Omondi Were ambaye ni Mkurugenzi wa Mazingira katika Kaunti ya Nakuru.

Miongoni mwa makosa watakayoshtakiwa nayo ni mauaji, kutotekeleza majukumu yao na kushindwa kuandaa ripoti ya athari za mazingira zilizosababishwa na mkasa huo. DPP amesema ameamuru Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi kuwakamata washukiwa na kwamba ofisi yake itahakikisha washukiwa wote wanafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.