array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta kukutana na Rais wa Shirikisho la Uswizi Alain Berset

Rais Uhuru Kenyatta kukutana na Rais wa Shirikisho la Uswizi Alain Berset

Rais Uhuru Kenyatta kukutana na Rais wa Shirikisho la Uswizi Alain Berset

Rais Uhuru Kenyatta Jumatatu wiki ijayo anatarajiwa kukutana na Rais wa Shirikisho la Uswizi, Alain Berset ambaye atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku mbili. Kulingana na Kitengo cha Habari za Ikulu, inayoongozwa na Msemaji Manoah Esipisu viongozi hao wawili watathmini jinsi watakavyoshirikiana katika kufanikisha Ajenda Nne Kuu za Rais za uzalishaji chakula, makao ya bei nafuu, ujenzi wa viwanda na huduma ya kimataifa ya matibabu.

Ziara ya Berset inapania kuimarisha uhusiano wa mataifa haya mawili. Kenya inategemea ushirikiano wa Uswizi kuiboresha sekta ya afya ili kuongeza nafasi za kupata dawa kwa magonjwa yasiyoambukiwa kama vile ugonjwa kisukari, saratani ya matiti, maradhi ya kupumua na magonjwa ya moyo na mishipa.

Masuala mengine yatakayojadiliwa kati ya Rais na Berset ni kuhusu uhamiaji na usalama katika  mataifa saba yaliyo chini ya shirika la IGAD, ambalo linaongoza mikakati ya kurejesha amani na utulivu katika taifa la Sudan Kusini.