array(0) { } Radio Maisha | Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi akosa kufika mahakamani kujibu mashtaka ya utumiaji mbaya wa ofisi

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi akosa kufika mahakamani kujibu mashtaka ya utumiaji mbaya wa ofisi

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi akosa kufika mahakamani kujibu mashtaka ya utumiaji mbaya wa ofisi

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Michael Kamau amekosa kufika mbele ya Mahakama ya Ufisadi kwa mara ya pili, huku akitaka rufaa yake isikilizwe katika Mahakama ya Juu. Kupitia wakili wake, James Orengo, Kamau ameitaka mahakama hiyo kusitisha kesi dhidi yake kuhusu utumiaji mbaya wa ofisi na ukiukaji wa sheria za ununuzi hadi Mahakama ya Juu itakapoisikiliza na kutoa uamuzi wa rufaa hiyo.

Hakimu Douglas Ogot ameelezwa kuwa waziri huyo wa zamani aliitaja rufaa hiyo kuwa ya dharura. Hata hivyo upande wa mashtaka umepinga ombi hilo ukisema Mahakama ya Rufaa iliitupilia mbali kesi hiyo na kuwapa nafasi kuendeleza. Aidha umesisitiza kwamba hakuna agizo la kumzuia Kamau kujibu mashtaka yanayomkabili.

Ikumbukwe Kamau alidai kuwa kesi hiyo ilitokana na njama ya mahasimu wake kumharibia jina. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wake Ijumaa wiki hii.