array(0) { } Radio Maisha | Gavana Sospeter Ojaamong' akana madai ya utumiaji mbaya wa ofisi

Gavana Sospeter Ojaamong' akana madai ya utumiaji mbaya wa ofisi

Gavana Sospeter Ojaamong' akana madai ya utumiaji mbaya wa ofisi

Saa chache baada ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji kuidhinisha kwamba Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong' afunguliwe mashtaka ya utumiaji mbaya wa ofisi na ukiukaji wa sheria za ununuzi wa mali ya umma, gavana huyo ameyakana madai hayo. Akizungumza na wanahabari mapema leo katika eneo la Budalang'i, Ojaamong amesema anafahamu kuhusu taarifa hizo kupitia vyombo vya habari. Kadhalika amesisitiza kwamba hakuna fedha zozote zilizopotea katika kaunti yake na kwamba malipo ya miradi yote iliyoendeshwa katika kaunti yake yalitolewa kwa kuzingatia sheria.

Vilevile amesema hatua hiyo ya DPP ni ya kisiasa na kuwafumba macho Wakenya kuhusu sakata mbalimbali zilizofichuliwa nchini, ikiwamo ya sukari iliyoingizwa nchini kimagendo.

Wengine walioshtakiwa naye ni Timothy Otieno Mboga, Benard Krade Yale, Lenadrd Wanda Obibira, Samuel Osieko Ombui, Allan Okweny Omachari, Edna Adhiambo Odoyo, Renish Achieng na Sebastian Hannlesleben. Haji ameidhinisha mashtaka hayo ambayo inaarifiwa yaliigharimu serikali ya kaunti hiyo kima cha shilingi milioni 20.