array(0) { } Radio Maisha | Takriban vibali elfu 18 vimesajiliwa na kukamatwa kwa watu 31

Takriban vibali elfu 18 vimesajiliwa na kukamatwa kwa watu 31

Takriban vibali elfu 18 vimesajiliwa na kukamatwa kwa watu 31

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i amehakikisha kuwa muda wa usajili na kupewa vibali kwa wafanyakazi ambao ni raia wa mataifa ya kigeni hautaongezewa.

Akizungumza alipokagua shughuli ya usajili katika Jumba la Nyayo, Matiang'i amesema kufikia sasa, takriban vibali elfu 18 vimesajiliwa na kukamatwa kwa watu 31 waliokuwa wakisubiri kusajiliwa kinyume na sheria.

Matiang'i amesema watalii, wanadiplomasia na wanafunzi wa kigeni ndio wanaoruhusiwa nchini bila vibali vya kazi. Vilevile ametishia kumfurusha yeyote ambaye hatakuwa amesajiliwa kufikia tarehe 23 mwezi huu na kuwakamata kwa watu fisadi wanaowatapeli wageni.

Ikumbukwe wizara hiyo ilitoa makataa ya miezi mitatu kuanzia tarehe 21 mwezi Mei hadi Julai 21.