array(0) { } Radio Maisha | IEBC yapanga kuhama kutoka Jumba la Anniversary

IEBC yapanga kuhama kutoka Jumba la Anniversary

IEBC yapanga kuhama kutoka Jumba la Anniversary

Tume ya Uchaguzi, IEBC inapania kuzihamisha ofisi zake kutoka jumba la Anniversary katikati ya Jiji la Nairobi. Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amesema hatua hiyo itasaidia kukabili uharibifu jijini wakati wa maandamano dhidi ya tume hiyo.

Ikumbukwe mwaka uliopita uharibifu mkubwa ulishuhudiwa jijini Nairobi wakati wa maandamano ya mara kwa mara ya wafuasi wa Muungano wa NASA waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsa ya siku mbili ya kutathmini uchaguzi mkuu uliopita linalofanyika kwenye Kaunti ya Mombasa, Chebukati aidha amesema maafisa wa tume hiyo wataelimishwa zaidi kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao ili kuhakikisha data za uchaguzi zinahifadhiwa vyema.

Wakati uo huo amefichua kwamba bodi ya IEBC itafanyiwa mabadiliko na kutakuwapo na ukaguzi wa maafisa wote wa tume hiyo ili kudumisha uwajibikaji kazini.