array(0) { } Radio Maisha | Katibu wa Wizara ya Vijana Lilian Omollo arejea rumande

Katibu wa Wizara ya Vijana Lilian Omollo arejea rumande

Katibu wa Wizara ya Vijana Lilian Omollo arejea rumande

Katibu wa Wizara ya Vijana, Lilian Omollo amerejeshwa katika Gereza la Wanawake la Lang'ata. Hatua hii inafuatia uchunguzi uliofanywa na Idara ya Upelelezi, DCI na kubainisha kuwa yu salama na hastahili kuendelea kulazwa hospitalini. Omollo amekuwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta tangu Mei 30, baada ya kuzirai alipokuwa akiingizwa katika rumande Langa'ta.

Wiki jana, barua kutoka hospitali hiyo ilimwomba jaji aliyekuwa akisikiliza kesi dhidi ya washukiwa hao kumruhusu Omollo kutohudhuria vikao kwani alikuwa akiugua.

Omollo ambaye ni miongoni mwa washukiwa zaidi ya arubaini wanaochunguzwa kwa ufujaji wa pesa katika Taasisi ya Kitaifa ya Huduma za Vijana NYS, amekuwa akishtumiwa vikali kwamba huenda anajifanya kuwa mgonjwa ndipo akwepe adhabu.

Mshukiwa mwingine, Lucy Ngirita mamaye Ann Ngirita anatibiwa katika hospitali iyo hiyo ya Kenyatta, kufuatia agizo la mahakama. Lucy Ngirita kupitia wakili wake, Cliff Ombeta aliwasilisha ombi akitaka aruhisiwe kutafuta matibabu alipoieleza mahakama kwamba anaugua.