array(0) { } Radio Maisha | Miguna Miguna akataliwa na bunge la Nairobi

Miguna Miguna akataliwa na bunge la Nairobi

Miguna Miguna akataliwa na bunge la Nairobi

Bunge la Kaunti ya Nairobi limepinga uteuzi wa Miguna Miguna kuwa naibu gavana wa Mike Mbuzi Sonko. Spika Beatrice Elachi amesema Gavana Sonko ameagizwa kufanya uteuzi upya. Elachi aidha ametoa mfano wa kipengee cha 78 cha katiba ambacho hakiruhusu mtu mwenye uraia wa mataifa mawili kuwania wadhifa wowote serikalini. 

Uteuzi huo uliofanywa na Sonko tarehe 16 Mei uliibua hisia mbalimbali ikizingatiwa alimtea mtu ambaye si mwanachama wa Jubilee.

Hata hivyo Sonko alisisitiza kwamba Miguna alifaa kwani angefanikisha vita dhidi ya watu fisadi. Miguna kwa upande wake alielezea kushanganzwa na uteuzi huo akisema Sonko hakumshauri kabla ya kumteua.