array(0) { } Radio Maisha | Swazuri ajitetea kuhusu utata wa ardhi ya Ruaraka

Swazuri ajitetea kuhusu utata wa ardhi ya Ruaraka

Swazuri ajitetea kuhusu utata wa ardhi ya Ruaraka

Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi, NLC, Mohamed Swazuri ameiondolea lawama ofisi yake kutokana na madai kwamba ililipa kima cha shilingi bilioni 3.2 kwa ardhi ya Ruaraka ambayo inamilikiwa na serikali wala si mtu binafsi. Akiwahutubia wanahabari, Swazuri amesema ardhi hiyo ambayo Shule ya Msingi ya Drive Inn na Shule ya Upili ya Ruaraka zimejengwa, ilikuwa mali ya mtu binafsi ndiposa serikali ikalazimika kuilipia baada ya kuitwaa.


Swazuri aidha amesisitiza kwamba umiliki wa ardhi hiyo tayari ulithibitishwa na kamati moja ya bunge mwaka 2012 vilevile kuthibitishwa na mahakama kwamba ni ardhi ya mtu binafsi.


Swazuri ambaye tayari amehojiwa na Maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, amesema yu tayari kuitetea tume yake kwani ilizingatia sheria katika kumlipa mmiliki wa ardhi hiyo fedha.