Rais Kenyatta awasimamsiha kazi makatibu wa wizara

Rais Kenyatta awasimamsiha kazi makatibu wa wizara

Rais Uhuru Kenyatta amewasimamisha kazi makatibu 15 wa wizara. Miongoni mwao ni Katibu wa Wizara ya Utalii, Fatuma Hersi, Katibu wa Uchukuzi na Miundo-msingi, John Mosonik, yule wa Leba Khadija Kassachoom, Katibu wa Madini, Mohamed Ibrahim Mahmoud, Katibu wa Ujenzi na Maendeleo Mijini, Aidah Munano, Katibu wa Mawasiliano na Uvumbuzi, Victor Kyalo, Katibu wa Mipango Irungu Nyakera na Fred Sigor wa Huduma za Maji.

Wengine ni Richard Ekai wa Urekebishaji Tabia, Katibu wa vyuo vya kiufundi, Jerotich Mwinzi, Partick Mwangi wa Uchukuzi, Katibu wa Huduma za Kijinisia, Mwanamaka Mabruki, Katibu wa Mashirikia, Ali Noor, Katibu wa Matangazo na huduma za simu, Sammy Itemere na Katibu wa Utamaduni, Joe Okudo. 

Katika taarifa, Mkuu wa Utumishi, Joseph Kinyua amesema licha ya kusimamishwa kwao, serikali ingali imebuniwa vilivyo na hakuna upungufu.