Mahakama ya Rufaa yabatilisha ushindi wa Gavana Mutua

Mahakama ya Rufaa yabatilisha ushindi wa Gavana Mutua

Gavana wa Machakos Alfred Mutua, ameapa kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa kubatilishi ushindi wake.

Akizungumza muda mchache baada ya uamuzi huo Mutua ameukashifu vikali akidai kuwa majaji walifeli kuangazia masuala muhimu yanayostahili kuangaziwa katika kesi za uchaguzi kukiwemo uhalali wa kura zilizopigwa.

Kwa upande wakili wa Mutua Wilfred Namu pia amekosoa uamuzi huo akidai kuwa majaji wamefeli kulezea kwa kina sababu za kubatilisha umuazi huo huku akiongeza kuwa huenda walitoa uamuazi wao kupitia madai ambayo hayakudhibitishwa mahakamani.

Wakati uo huo aliyekuwa mshindani wake Wavinya Ndeti amabye aliwasilisha kesi hiyo amesema kuwa yu tayari kukabiliana na Mutua katika mahakama ya Juu haku akiirai Tume ya Uchaguzi, IEBC kuanda uchaguzi huru wa haki iwapo uchaguzi huo utarudiwa tena. Vilevile amelezea imani yake ya kuibuka na ushindi wakati wa marudio ya kura hizo.

Mahakama ya Rufaa mapema leo imebatilisha ushindi wa Gavana Mutua na kutaja kuwa hakuchaguliwa kihalali huku kuiamrisha Tume ya Uchaguzi IEBC kuandaa uchaguzi mwengine kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Gavana huyo amesisitiza kuwa bado yungali mamlakani na kuwaahidi wakazi wa kaunti ya Machakos kuwa ataendelea kuwahudumia vilivyo na kuwa uamuzi huo hautayumbisha amza yake ya kuwania urais mwaka