Kenya Power yasitisha huduma City Hall

Kenya Power yasitisha huduma City Hall

Kampuni ya Kusambaza Kawi- Kenya Power  imesitsha huduma za umeme katika makao makuu ya Kaunti ya Nairob kufuatia deni kubwa inalodai.

Kwa  mujibu wa taarifa kutoka Kenya Power, Kaunti ya Nairobi inadaiwa shiling bilioni 990 kupitia akaunti zaidi ya elfu tano za umeme.

Kwa muda sasa kumekuwa na mvutano kuhusu deni hilo huku mwaka uliopita serikali hiyo ikielekea mahakamani ikilalamikia deni la shilingi milioni 543 ililokuwa ikidaiwa na Kenya Power. Hata hivyo kwa sasa, huduma zilizositishwa ni za akaunti mbili ambazo ni muhimu kwa utoaji huduma za Kaunti ya Nairobi.