array(0) { } Radio Maisha | Wabunge waidhinisha makadirio ya bajeti

Wabunge waidhinisha makadirio ya bajeti

Wabunge waidhinisha makadirio ya bajeti

Wabunge mapema Jumatano wameahirisha vikao vyao vya kawaida ili kutoa fursa ya kujadiliwa kwa ripoti ya Kamati ya Bajeti ya iliyoidhinisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/ 2019 itakayogharimu shilingi trilioni 3.074.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kimani Ichungwa imeitengea Serikali ya Kitaifa shilingi trilioni 1.676, idara ya mahakama shilingi bilioni 17.76, bilioni 46 zikitengewa mabunge yote mawili huku serikali za kaunti zikipata shilingi biioni 374.

Aidha kwa mujibu wa makadirio hayo, serikali inalenga kutumia shilingi trilioni 1.73 kutokana na kodi inayokusanywa kutoka kwa wananchi huku shilingi bilioni 47.03 zikiwa ufadhili wa mataifa ya kigeni na mikopo kutoka taasisi mbalimbali.

Hata hivyo kamati hiyo imependekeza kuwa ni sharti mairadi yote ambayo itatekelezwa na serikali na kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 1 ipigwe msasa na bunge kabla ya kuidhinishwa na kutekelezwa.

Aidha imesema vikao vya umma kutoa maoni yao kuhusu mipango ya matumizi ya fedha ya serikali ni sharti viandaliwe mapema ili kuipa nafasi mwafaka ya kutathmini mapendekezo hayo kwani muda uliowekwa sasa hautoshi.

Ripoti hiyo imetiliwa mkazo na Mbunge wa Kitui ya Kati, Benson Molu aliyependekeza kuwa wizara ambazo zimekumbwa na utata wa utumiaji mbaya ya fedha kupunguziwa mgao wake huku akisisitiza haja ya kukamilishwa kwa miradi ambayo imechukua muda mrefu kumalika kabla ya kuanzishwa kwa miradi mipya.